Posts

Showing posts with the label Michezo

NEWS

**Exploring Zanzibar: The Intriguing Isle with a Touch of Merriment.

Image
 Welcome to Zanzibar, an island paradise that appears as though it's been plucked from the pages of a fairy tale. Situated off the coast of Tanzania, Zanzibar offers more than just breathtaking beaches and crystal-clear waters. It's a place where history, enigma, and a touch of whimsy converge in a tropical concoction. Prepare yourself as we delve into some entertaining, enigmatic, and downright eccentric facts about this captivating destination! 1. The Spice Island: Beyond Aroma Zanzibar is commonly referred to as the "Spice Island"due to its extensive history of spice cultivation. However, did you realize that the island’s spice trade has resulted in some culinary peculiarities? For example, locals have been known to incorporate cloves into their coffee—yes, cloves! While it may sound peculiar, it provides an aromatic punch that could potentially convert you into a spice aficionado. Just refrain from requesting a clove-infused latte at your neighborhood café—unless ...

Cristiano Ronaldo asema anahisi 'kusalitiwa' na Manchester United

Image
Nyota wa Manchester United Cristiano Ronaldo anahisi kusalitiwa na Manchester United  na kwamba analazimishwa kuondoka katika klabu hiyo. Ronaldo aliahidi mwezi Agosti kwamba atatowa toleo lake la maisha ya Ulaya kama alivyotumai. Mchezaji huyo wa miaka mingi wa Ureno sasa amevunja kimya chake katika mahojiano na Piers Morgan katika runinga ya TalkTV Klabu ya Manchester United imeombwa kutoa tamko ili kujibu madai hayo ya Ronaldo. United ambayo iliichapa Fulham 2-1 siku ya Jumapili, iko katika nafasi ya tano katika ligi ya Uingereza chini ya ukufunzi wa Ten Hag katika msimu wake wa kwanza. Alipoulizwa iwapo uongozi wa United ulikuwa unajaribu kumfukuza katika klabu hiyo, Ronaldo alisema: "Ndiyo, si tu kocha [Erik ten Hag], lakini pia watu wengine wawili au watatu katika klabu. Nilihisi kusalitiwa. Alipoulizwa tena kama viongozi wakuu wa klabu walikuwa wakijaribu kumtimua, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alisema:   "Sijali.  Watu wanapaswa kusikiliza ukweli. "Ndio, ...

Kwanini Qatar inatuhumiwa 'kujitakasa kimichezo'

Image
Kombe la Dunia linakaribia kuanza lakini utata unaohusu haki za wapenzi wa jinsia moja, haki za wafanyakazi na uhuru wa kujieleza nchini Qatar unaendelea.   Hii imesababisha madai kuwa nchi hiyo inajaribu "kusafisha" sifa yake kwa kuandaa mashindano hayo.   Lakini kujitakasa kimichezo ni  nini na je neno hili ni sahihi?

Kauli ya MO Dewji baada ya Yanga kushinda dhidi ya Club Africain

Image
“Hongera sana mtani, umeifanya umeifaharisha Tanzania. Karibu kwenye michuano mikubwa.” Ameandika Rais wa heshima wa Simba SC, Mohammed Dewji ‘Mo’ amesema siku moja baada ya Yanga kufuzu hatua ya makundi kwa kumtandika Club Africain bao 1-0 nchini Tunisia. Baada ya ushindi huo, Yanga sasa inasubiri droo ya hatua ya makundi itakayofanyika Jumatano ya Novemba 16 Cairo Misri, kuona itapangiwa na timu zipi katika hatua hiyo.

Kombe la Dunia 2022: Kauli ya balozi wa kombe la dunia Qatar kuhusu wapenzi wa jinsia moja 'haikubaliki'

Image
Shirika la haki za binadamu la Human right watch limesema kauli ya Balozi wa Kombe la Dunia Qatar kuhusu mapenzi ya jinsia moja kuharibu fikra "ina madhara na haukubaliki". Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Qatar Khalid Salman aliliambia shirika la utangazaji la Ujerumani, ZDF kwamba watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wanaohudhuria mashindano hayo wanapaswa "kutii sheria zetu". Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria nchini Qatar kwa sababu inachukuliwa kuwa ni kinyume cha maadili chini ya sheria ya Kiislamu ya Sharia. Salman alisema: "(Mapenzi ya jinsia moja) ni haram. Unajua nini maana ya haram (iliyokatazwa)?" Alipoulizwa kwa nini ni haram, aliongeza: "Mimi si Muislamu mwenye msimamo mkali lakini kwa nini ni haram? Kwa sababu inaharibu akili." Mahojiano hayo, ambayo ni sehemu ya filamu iliyopangwa kutangazwa siku ya Jumanne, yalisimamishwa na afisa aliyepinga. Rasha Younes, mtafiti mkuu wa haki za watu wa mapenzi ya jinsi...

Rais wa Yanga, Eng. Hersi ampatia Pikipiki Kijana aliyeokoa Watu 24 ajali ya Ndege, GSM nao watoa Milioni 5

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameagiza Kijana Majaliwa Jackson aliyehusika kuwaokoa Watu 24 kwenye ajali ya ndege iliyotokea Bukoba siku jana atafutiwe kazi kwenye Jeshi la Uokozi. Agizo hilo lililotolewa na Rais Samia kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambapo ameagiza Kijana Majaliwa Jackson akabidhiwe kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na atafutiwe nafasi kwenye Jeshi la Uokozi ili Kijana huyo apate mafunzo zaidi kutokana na ujasiri wake huo kisha aingie kwenye Jeshi hilo ambalo linahitaji ujasiri aliouonesha. Sasa leo Novemba 8, 2022 Rais wa Yanga Hersi akiwa Tunisia amewasiliana na Haji Manara na kuahidi kijana huyo kumpatia Pikipiki mpya itakayomsaidia kwenye shughuli zake ikiwa kama kumfariji kwa kile ali chokifanya katika ajali ya Ndege iliyoanguka Ziwa Victoria.

Hersi awaomba radhi mashabiki wa yanga

Image
Rais wa Yanga SC Hersi Said ameongea kwa mara ya kwanza kuhusu sare ya 0-0 ya Yanga SC dhidi ya Club Africain ya Tunisia ukiwa ni mchezo wa mkondo wa kwanza wa mtoano wa Kombe la Shirikisho Afrika uliyochezwa November 2 2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa. Hersi ameomba radhi mashabikiwa Yanga SC na kuwapa pole kutokana na kutopendezwa na matokeo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi maoni yao huku akiwaomba wapuuzie kauli yake inayotumika kuwakejeli mashabiki wa Yanga. “Baada ya mchezo huo kuisha tulipata maoni ya wanachama na wapenzi wetu, sisi kama viongozi tumeyapokea kwa mikono miwili na kamati yangu ya utendaji” “Maoni yenu ni muhimu sana katika kujenga timu yetu, kupitia hapo wapo baadhi ya watu wasioitakia mema club yetu wakitumia kauli yangu niliyoitoa wakati nazungumza na viongozi wa matawi jijini Mwanza wakiitumia kauli ile kuwakejeli baadhi ya mashabiki nataka niwahakikishie uongozi wenu umekuwa sikivu sana” Mashabiki wa Yanga hawakuridhishwa na kiwango cha timu yao dhidi ya Clu...

FIFA yaonya Siasa kombe la Dunia

Image
Shrikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu ‘FIFA’ limezionya timu zote zitakazoshiriki Kombe la Dunia nchini Qatar juu ya viashiria vyovyote katika kila vita vya kiitikadi au kisiasa vinavyoendelea katika baadhi ya mataifa. Rais wa FIFA, Gianni Infantino na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Fatma Samoura wametuma barua kwa timu hizo wakipiga vita masuala hayo.  Baadhi ya ligi kama EPL na Laliga zilizonekana zikilitetea Taifa la Ukraine. Katika barua hiyo imeeleza kuwa imekuwa ni maendeleo ya Kombe la Dunia iliyogubikwa na wasiwasi kuhusu mateso ya wafanyakazi wahamiaji wanaolipwa mshahara mdogo, kujenga miundombinu katika Taifa dogo la Ghuba na sheria za kibaguzi zinazoharamisha mahusiano ya watu wa jinsia moja. “Tafadhali, sasa tuzingatie soka!” Infantino na Samoura waliyaandikia mataifa 32 ya soka yatakayoshiriki Kombe la Dunia.

Sababu ya mshambuliaji wa Tanzania kung’ang’aniwa na klabu za West Ham, Everton na Burnley England

Image
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta anang'ang'aniwa na klabu tatu za England, taarifa za vyombo vya habari nchini Uingereza zinasema. Tetesi zinasema nyota huyo anatafutwa na West Ham United, Everton na Burnley. Samatta, 25, maarufu kwa Watanzania kama Samagoal ameng'aa sana akichezea klabu ya KRC Genk nchini Ubelgiji. Amefungia klabu hiyo mabao 11 katika mechi 16 ambazo amewachezea msimu huu, nusu ya mabao hayo akiyafunga barani Ulaya. Taarifa za kumhusisha Samatta na klabu ya Everton zimetoka kwa mtandao wa hitc.com, mmoja wa mitandao ambayo imeibukia kuwa maarufu kwa taarifa za wachezaji na kuhama kwao. Kwa nini anahusishwa na Everton? Samatta, mwenye kimo cha futi 5 inchi 11, amefunga mabao sita katika ligi ndogo ya klabu barani Ulaya, Europa League, na ni hapo ameanza kuonekana na klabu za England. Mnamo 23 Agosti 2018 Samatta, alifunga 'hat-trick' dhidi ya Brøndby IF katika Europa League kwenye mechi ambayo walishinda 5...

Messi aongeza mtoto wa tatu

Image
Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi na mkewe Antonella Roccuzzo wamefanikiwa kupata mtoto wao wa tatu wa kiume.  Hilo amethibitisha Messi kupiia mtandao ake w Instagram kwa kuweka picha hiyo hapo chini na kuandika, “Karibu Ciro! Asante Mungu kila kitu kilikwenda kikamilifu. Mama na mtoto wote wapo salama. Tunafuraha kubwa sana!!!!! ❤❤.”  Mtoto huyo tayari amepewa jna la Ciro ambapo anaungana na kaka zake wawili akiwemo Mateo (2) na Thiago (5).  Wakati huo huo mpinzani wa Messi, Cristiano Ronaldo ana watoto wanne, wakiwemo wwili mapacha.  kutokana na ujio wa mtoto huyo Messi amepewa mapumziko na timu yake hivyo hatakuwepo katika mchezo wa usiku wa leo ambao Barcelona watacheza na Malaga katika mechi ya La Liga na nafasi yake imepangwa kuchukuliwa na mchezaji Yerry Mina.

Christiano Ronaldo mchezaji bora wa kiume 2017

Image
Cristiano Ronaldo ameshinda taji la shirikisho la soka duniani FIFA la mchezaji bora wa kiume wa kandanda mwaka huu kwa mara ya pili mtawalia. Tuzo hiyo kwa mchezaji bora mwanamke aliinyakuwa mchezaji wa Uholanzi Lieke Martens, anayeichezea Barcelona. Mchezaji huyo kutoka Ureno, amefunga mabao 44 katika mechi 48 alizoshiriki katika mwaka, kuiwakilisha nchi yake pamoja na timu anayoichezea ya Real Madrid aliyochangia kufanikisha ushindi wake katika mataji ya ligi ya Uhispania La Liga na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Aliwashinda Lionel Messi wa Barcelona na mchezaji ghali zaidi duniani anayechezea Paris St-Germain, Mbrazil Neymar. Messi alimpigia kura mwenzake wa Barcelona Luis Suarez naye Ronaldo alimpigia mwenzake wa Real - Luka Modric. Meneja wa England Gareth Southgate alimpigia kura Ronaldo. Ufanisi kwa Cristiano Ronaldo Ulikuwa ni mwaka mwingine wa ufanisi kwa Ronaldo, aliyekuwa ameshinda tuzo ya kwanza ya Mchezaji Bora wa Fifa kwa mwaka 2016. Aliendeleza ufanisi w...

Popular posts from this blog

"Whispers of the Savannah: The Enchanting Life of Tanzania's Hadzabe Tribe"

Hatua za kufuata unapopoteza kitambulisho cha Taifa

The Secret Guardians of Tanzania's Wild: Unearthing the Myths of Hidden Trolls