NEWS

**Exploring Zanzibar: The Intriguing Isle with a Touch of Merriment.

Image
 Welcome to Zanzibar, an island paradise that appears as though it's been plucked from the pages of a fairy tale. Situated off the coast of Tanzania, Zanzibar offers more than just breathtaking beaches and crystal-clear waters. It's a place where history, enigma, and a touch of whimsy converge in a tropical concoction. Prepare yourself as we delve into some entertaining, enigmatic, and downright eccentric facts about this captivating destination! 1. The Spice Island: Beyond Aroma Zanzibar is commonly referred to as the "Spice Island"due to its extensive history of spice cultivation. However, did you realize that the island’s spice trade has resulted in some culinary peculiarities? For example, locals have been known to incorporate cloves into their coffee—yes, cloves! While it may sound peculiar, it provides an aromatic punch that could potentially convert you into a spice aficionado. Just refrain from requesting a clove-infused latte at your neighborhood cafĂ©—unless ...

Cristiano Ronaldo asema anahisi 'kusalitiwa' na Manchester United


Nyota wa Manchester United Cristiano Ronaldo anahisi kusalitiwa na Manchester United  na kwamba analazimishwa kuondoka katika klabu hiyo.


Ronaldo aliahidi mwezi Agosti kwamba atatowa toleo lake la maisha ya Ulaya kama alivyotumai.


Mchezaji huyo wa miaka mingi wa Ureno sasa amevunja kimya chake katika mahojiano na Piers Morgan katika runinga ya TalkTV


Klabu ya Manchester United imeombwa kutoa tamko ili kujibu madai hayo ya Ronaldo.
United ambayo iliichapa Fulham 2-1 siku ya Jumapili, iko katika nafasi ya tano katika ligi ya Uingereza chini ya ukufunzi wa Ten Hag katika msimu wake wa kwanza.


Alipoulizwa iwapo uongozi wa United ulikuwa unajaribu kumfukuza katika klabu hiyo, Ronaldo alisema: "Ndiyo, si tu kocha [Erik ten Hag], lakini pia watu wengine wawili au watatu katika klabu. Nilihisi kusalitiwa.


Alipoulizwa tena kama viongozi wakuu wa klabu walikuwa wakijaribu kumtimua, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alisema:
 "Sijali. Watu wanapaswa kusikiliza ukweli.

"Ndio, nilihisi kusalitiwa na nilihisi kama watu wengine hawanitaki hapa, sio mwaka huu tu bali mwaka jana pia."

Ronaldo anasema ‘hamuheshimu’ Ten Hag

Ronaldo hajachezeshwa kutokana na magonjwa yasiojulikana tangu alipoingoza United katika kushindwa 3-1 na Aston Villa tarehe sita mwezi Novemba.


Aliondolewa kwenye mechi ya Ligi ya Premia huko Chelsea mwezi uliopita na Ten Hag baada ya kukataa kuingia kama mchezaji wa akiba dhidi ya Tottenham siku tatu zilizopita.


"Sina heshima naye kwa sababu haonyeshi heshima kwangu," Ronaldo alimwambia Morgan. "Ikiwa huniheshimu, sitawahi kukuheshimu."


Mahojiano hayo yataonyeshwa kwa siku mbili za usiku wa Jumatano na Alhamisi.
Ronaldo pia anazungumza na Morgan kuhusu kufiwa na mtoto wake wa kiume mwezi Aprili na jinsi alivyoguswa na heshima aliyopewa na mashabiki wa Liverpool kwenye mechi dhidi ya United Uwanjani Anfield siku chache baadaye.


Mahojiano yote ni ya dakika 90 lakini Morgan ameandika toleo kwenye gazeti la Sun ambalo ni wazi dharau aliyonayo Ronaldo kwa jinsi alivyoikuta United tangu aliporejea klabuni huko huku mashabiki wakifurahia hatua hiyo Agosti 2021.


"Nadhani mashabiki wanapaswa kujua ukweli," anasema. "Naitakia mema klabu hii . Hii ndiyo sababu nimekuja Manchester United.


"Tangu [meneja wa zamani] Sir Alex [Ferguson] alipoondoka, sijaona mabadiliko yoyote katika klabu. Hakuna kilichobadilika.


"Ninaipenda Manchester United, ninawapenda mashabiki, daima wapo upande wangu. Lakini kama wanataka kufanya hivyo tofauti... inabidi wabadilishe mambo mengi."


Ronaldo anasema mtazamo wake kuhusu klabu hiyo unafanana na Ferguson, ambaye alikuwa muhimu katika kurejea kwake Old Trafford kutoka Juventus ilipoonekana huenda akajiunga na Manchester City.


"Anajua zaidi ya mtu yeyote kwamba klabu haiko kwenye njia inayostahili kuwa," aliongeza Ronaldo.


"Anajua. Kila mtu anajua. Watu ambao hawaoni hilo ... ni kwa sababu hawataki kuona; wao ni vipofu."

Ronaldo hakuwahi 'kumjua' Rangnick

Mchezaji mwenza wa zamani wa Ronaldo Ole Gunnar Solskjaer alikuwa meneja wa United wakati Mreno huyo aliporejea klabuni hapo kabla nafasi yake kuchukuliwa na Ralf Rangnick na kisha kocha wa sasa Ten Hag.

Kuhusu Rangnick, Ronaldo alisema: "Kama hujawahi kuwa, utawezaje kuwa bosi wa Manchester United? Sijawahi hata kumsikia."

Wayne Rooney amekosoa tabia ya mchezaji mwenzake wa zamani wa United Ronaldo msimu huu na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno pia alimkosoa mshambuliaji huyo wa zamani wa Uingereza.

"Sijui kwanini ananikosoa sana... labda kwa sababu alimaliza kucheza soka na anaona bado mimi nacheza kwa kiwango cha juu," alisema Ronaldo.

"Sitasema kwamba ninaonekana bora kumliko yeye. Kitu ambacho ni kweli ..."

Comments

Popular posts from this blog

"Whispers of the Savannah: The Enchanting Life of Tanzania's Hadzabe Tribe"

Hatua za kufuata unapopoteza kitambulisho cha Taifa

The Secret Guardians of Tanzania's Wild: Unearthing the Myths of Hidden Trolls