**Exploring Zanzibar: The Intriguing Isle with a Touch of Merriment.
![Image](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiRLxv47xituEIBCsdJuo_Dzeha7dLpw3gnahpE7Cgqbvh5L3nE0FQfCYvOniDLymM3EXYKhwaxRvA48BoLwz7zzCxxzdTyIcvX4CZUilA3ilf2cRu29H5WS8AWl_jN8WuN2QDaqoefRpN2JDtmTRbQeXsoRUk1Jqhcfk3p7N13t-r0bMHBLmWyDC3KtHWv/w400-h299/images.jpg)
Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Qatar Khalid Salman aliliambia shirika la utangazaji la Ujerumani, ZDF kwamba watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wanaohudhuria mashindano hayo wanapaswa "kutii sheria zetu".
Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria nchini Qatar kwa sababu inachukuliwa kuwa ni kinyume cha maadili chini ya sheria ya Kiislamu ya Sharia. Salman alisema: "(Mapenzi ya jinsia moja) ni haram. Unajua nini maana ya haram (iliyokatazwa)?"
Alipoulizwa kwa nini ni haram, aliongeza: "Mimi si Muislamu mwenye msimamo mkali lakini kwa nini ni haram? Kwa sababu inaharibu akili." Mahojiano hayo, ambayo ni sehemu ya filamu iliyopangwa kutangazwa siku ya Jumanne, yalisimamishwa na afisa aliyepinga.
Rasha Younes, mtafiti mkuu wa haki za watu wa mapenzi ya jinsia moja (LGBT) wa Human Rights Watch, alisema: "Maoni ya Salman kwamba mvuto wa watu wa jinsia moja ni 'uharibifu wa akili' ni hatari na haikubaliki.
"Kushindwa kwa serikali ya Qatar kukabiliana na taarifa hizi za uwongo kuna athari kubwa kwa maisha ya wapenzi wa jinsia moja wa Qatar, kuanzia kuchochea ubaguzi na unyanyasaji dhidi yao hadi kuhalalisha kuwaweka kwenye desturi za uongo zinazofadhiliwa na serikali."
Kuna wasiwasi kuhusu jinsi wapenzi wa jinsia moja na wale waliobadilisha jinsia (LGBTQ+) wanavyoshughulikiwa nchini Qatar, ambapo mahusiano ya watu wa jinsia moja ni kosa la jinai, anayebainika anapigwa adhabu ya kuanzia faini hadi hukumu ya kifo.
Waandaaji wa Kombe la Dunia nchini humo wamesema "kila mtu anakaribishwa" kuzuru nchi hiyo kutazama mechi za mashindano hayo na kudai hakuna atakayebaguliwa.
Hata hivyo, mtendaji mkuu wa Qatar 2022 Nasser al Khater amesema serikali haitabadilisha sheria zake kuhusu mapenzi ya jinsia moja, na kuwataka wageni "kuheshimu utamaduni wetu".
Jimbo la Ghuba, ambako Kombe la Dunia litafanyika kuanzia tarehe 20 Novemba hadi 18 Disemba, pia limekosolewa kwa rekodi yake mbaya ya haki za binadamu dhidi ya wafanyakazi wahamiaji.
Fifa hivi majuzi iliyaandikia mataifa yanayoshiriki mashindano hayo na kuyataka "kujielekeza kwenye soka" badala ya mazonge mengine kuelekea mashindano hayo.
Barua hiyo, ambayo ilitiwa saini na rais wa Fifa, Gianni Infantino, ilikosolewa na wanaharakati wa Human Rights Watch, Amnesty International na LGBTQ+ nchini Uingereza na Wales, huku vyama 10 vya soka vya Ulaya - vikiwemo vya Engalnd na Wales - vilisema "haki za binadamu ni za ulimwengu wote na zinatumika kila mahali".
Hata hivyo, Conmebol, shirikisho la kandanda la Amerika Kusini, linasema ni "wakati wa kuacha mabishano".Kundi la kampeni la LGBTQ+ All Out lilitoa wito kwa Fifa "kukomesha ukimya na unafiki" kufuatia maoni ya Salman.
Katika maandamano nje ya jumba la makumbusho la Fifa mjini Zurich, msemaji kutoka All Out alisema: "Hii inakuja siku chache baada ya All Out na wengine kuwasilisha ushuhuda kutoka kwa LGBT+ Qatar kuhusu utekaji nyara, kuwekwa kizuizini bila kufunguliwa mashtaka, mateso na mazoea ya kubadili dini yanayofanyika katika wiki za hivi karibuni.
"Lakini rais wa Fifa Infantino bado anasema kwamba kila mtu atakaribishwa kwenye Kombe la Dunia.“Zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya kombe la dunia kuanza, ni wakati wa Fifa kuacha kuangalia pembeni na kuwajibika."Ni wakati wa Fifa kukomesha ukimya na unafiki.
Hatimaye ni wakati wa haki za binadamu kutazamwa...Ulimwengu unatazama."
Hivi majuzi Human Rights Watch ilitoa ripoti ikisema kwamba vikosi vya usalama vya Qatar vinaendelea kuwakamata raia ambao wanajishughulisha na mapenzi ya jinsia moja na waliobadili jinsia, wakati mwingine wakiwalazimisha kubadili dini.
Serikali ya Qatar imesema ripoti hiyo ina madai ya uongo.Mkurugenzi wa mawasiliano na mambo ya nje wa LGBTQ+ Stonewall Robbie de Santos alisema haki za binadamu "zilikuwa zinapuuzwa na kudharauliwa".
Akiongea na Sport Today ya BBC World Service, aliongeza: "Inashangaza na kukatisha tamaa mamlaka ya Qatar imetoa hakikisho kwa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa kuhusu kuheshimu haki za binadamu wakati wa mashindano hayo na kutoa ahadi kwa maendeleo ya kijamii, na kile tunachokiona ni kwamba ahadi hizo hazitekelezwi.
"Ndio maana ni muhimu sana kwamba sisi sote tusikilize na kufuatilia mashindano na kujua kwamba mpira wa miguu ni mchezo wa kila mtu, na kwamba sote tunazungumza."BBC Sport imewasiliana na Fifa na kamati ya maandalizi ya Kombe la Dunia kwa maoni yao.
Comments
Post a Comment