NEWS

**Exploring Zanzibar: The Intriguing Isle with a Touch of Merriment.

Image
 Welcome to Zanzibar, an island paradise that appears as though it's been plucked from the pages of a fairy tale. Situated off the coast of Tanzania, Zanzibar offers more than just breathtaking beaches and crystal-clear waters. It's a place where history, enigma, and a touch of whimsy converge in a tropical concoction. Prepare yourself as we delve into some entertaining, enigmatic, and downright eccentric facts about this captivating destination! 1. The Spice Island: Beyond Aroma Zanzibar is commonly referred to as the "Spice Island"due to its extensive history of spice cultivation. However, did you realize that the island’s spice trade has resulted in some culinary peculiarities? For example, locals have been known to incorporate cloves into their coffee—yes, cloves! While it may sound peculiar, it provides an aromatic punch that could potentially convert you into a spice aficionado. Just refrain from requesting a clove-infused latte at your neighborhood cafĂ©—unless ...

Wakala wa majengo (TBA) washindwa kubomoa jengo la TANESCO


Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wameshindwa kubomoa jengo la Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lililopo eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam, ndani ya muda waliopewa na serikali kufanya hivyo. 

Jumatatu wiki hii, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mwasiliano, Joseph Nyamuhanga aliiagiza TBA kuhakikisha kwamba, ifikapo Februari Mosi mwaka huu wawe wamebomoa jengo hilo. Lakini hadi jana, jengo hilo lilikuwa bado halijabomolewa. 

Maagizo hayo yalipokelewa vizuri na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa TANESCO, Khalid James ambaye aliihakikishia serikali kwamba, hadi kufika jana ambayo ni siku ya mwisho, jengo hilo lingekuwa limebomolewa. 

Licha ya kuwa wakafanyakazi wa TBA wanaendelea na mchakato wa kubomoa jengo hilo, lakini hawapo katika nafasi ya kukamilisha ubomoaji huo siku za usoni. 

Wakieleza sababu za kushindwa kukamilisha ubomoaji huo, TBA wamesema kuwa, changamoto kubwa ni eneo lilipo jengo hilo ambapo panafanya shughuli za ubomoaji kuwa ngumu. 

Aidha, wameeleza kwamba, changamoto ya jengo hilo kuwa pembezoni mwa barabara kuu ambayo muda wote inatumika na shughuli nyingine jirani na jengo hilo zinaendelea imekuwa kikwazo. 

TBA wamesema wana uhakika kwamba, hadi kumalizika kwa wiki ijayo, watakuwa wamekamilisha ubomoaji huo. 

Rais Dkt Magufuli aliagiza jengo hilo kubomolewa kutokana na kuwa katika hifadhi ya barabara ili kupisha mradi wa ujenzi wa barabara ya juu.

Comments

Popular posts from this blog

"Whispers of the Savannah: The Enchanting Life of Tanzania's Hadzabe Tribe"

Hatua za kufuata unapopoteza kitambulisho cha Taifa

The Secret Guardians of Tanzania's Wild: Unearthing the Myths of Hidden Trolls